Featured

    Featured Posts

Viongozi 73 Wasulubiwa Baraza la Maadili




JUMLA ya viongozi 73 wameshafikishwa mbele ya Baraza la Maadili katika kipindi cha mwaka 2010/11 hadi 2014/15.
Takwimu hizo zilitolewa bungeni jana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Fakharia Shomar Khamis (CCM),
Katika swali lake Mbunge huyo alitaka kujua idadi ya viongozi ambao ahadi sasa wameshafikishwa Sekretarieti ya Viongozi wa Umma kutokana na ukiukwaji wa maadili.
Mkuchika alisema viongozi hao walifikishwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo kushindwa kutoa tamko la rasilimali na madeni, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa tamko la uongo, kutotamka maslahi ya mkataba na Serikali na kutotamka zawadi.
“Kati ya malalamiko 73 yaliyofikishwa mbele ya Baraza, viongozi 18 hawakupatikana na hatia, 29 walipatikana na hatia na kupewa adhabu mbalimbali,” alisema.
Alisema watumishi 14 walipewa onyo, 10 walipewa onyo kali, wanne walipewa onyo na tahadhari na kiongozi mmoja alitozwa faini.
“Malalamiko 26 yaliyobakia yako kwenye hatua mbaalimbali ikiwemo malalamiko 17 ambayo yameahirishwa kusikilizwa na Baraza.
“Malalamiko matatu yanasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kufuatiwa walalamikiwa kuomba kupinga uamuzi mdogo wa Baraza wa kuendelea kuwachunguza,” alisema.
Mkuchika alisema Baraza limakubali lalamiko moja liendelee katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
“Malalamiko matano yamekamilika na taarifa yake imewasilishwa kwenye mamlaka husika kwa utekelezaji wa mapendekezo ya Baraza la Maadili,” alisema.

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

.....


Powered by Blogger.

Translate

Total Pageviews

Copyright © HABARI ZA LEO | Designed By Code Nirvana