Binadamu tuliumbwa kuishi
katika misingi ya ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa
porini leo naomba kusema kutoka moyoni mwangu.. Najua kabisa nina wazazi
wangu ndugu zangu na zaidi sana Mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa
kamwe sintowasahau katika kuta za moyo wangu katika kipindi changu
kigumu nilichopitia mlikuwa nembo namboni kubwa katika kuokoa maisha
yangu...
Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu.
Nakumbuka sana mlipojitoa
kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili
yangu,mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na
namshukuruu mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi
na moja ya sababu ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha
yangu.
Leo hii tarehe 25.5.2015
napenda kusema kwa umma na zaidi kwa Mungu wangu kuwa nawathamini
nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote mliyofanya juu yangu.
Nawaombea kwa Mungu
muendelee na moyo huo huo kwani naamini kuna wengi bado wanawategemea
ili kukomboa maisha yao kwa wakati aliyopanga mungu
Hata kitabu cha dini
kilisema kuwa "huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu
yako unayemuona" najua siku moja tutaishi kama zamani.. Ahsanteni
Kajala ameandika hayo
kwenye ukursa wake kwenye mtandao picha wa Instagram mara baada ya
kuweka picha hizo hapo juu ya Wema Sepetu na ya Petitman.Michango ya
wengi kwenye andiko hili, wamewataka Wema na Kajala muda umefik sasa
wayamalize
Post a Comment