Mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil, Marta Vieira da Silva
Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil Marta Vieira da Silva almaarufu
Marta ameweka historia ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la
dunia la wanawake baada ya kufikisha mabao 15.
Marta
amefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa
penati kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya korea kusini ambapo Brazili
waliibuka kidedea kwa mabao 2-0.
Ushindi huo umeifanya Brazil kuwa vinara wa kundi E, Baada ya Hispania na Costa Rica kwenda sare ya kufungana 1-1.
Mshambuliaji
huyu ameichezea timu ya taifa jumla ya michezo 137 akiwa kafunga mabao
93. Kwa sasa Marta ni mchezaji wa klabu ya Rosengard FC ya Sweden.
Post a Comment