Si Diamond pekee anayenufaika na muziki wake – hata madensa wake pia.
Diamond amesema madansa wake wanne tayari wamefanikiwa kujenga nyumba zao kutokana na kipato wanachopata.
Akiongea na gazeti la Mwanaspoti, staa huyo amesema amekuwa akiwashauri madansa wake mambo mazuri ya kimaisha ili kuwajenga.
“Ni
kama kaka zangu na ninawapenda sana kwani tumetoka nao mbali na wanajua
kuwa tunafanya kazi pamoja kutengeneza maisha hivyo ni kama ndugu zangu
na tunasaidiana kwenye kila jambo ukizingatia kuwa kile tunachokipata
tunagawana,” alisema Diamond.
“Kwa
kweli najitahidi sana kuwaambia hasa kuhusiana na masuala ya kimaisha,
nahusika katika maisha yao ya kila siku na nijuavyo mimi nikikosea tu
mmoja akapotea kundi langu litakuwa limeharibikiwa maana kila mtu
namtegemea kwa upande wake. Kwa sasa wamejenga nyumba zao na wanaendelea
vizuri kimaisha hilo ndilo sharti langu lazima wafanye mambo ya
maendeleo kwa kile tunachokipata.”
Post a Comment