Q-Chief
amedai kuwa ni muhimu jitihada zikafanyika na wadau mbalimbali ili
kumuokoa TID kutoka kwenye dimbwi la matumizi ya madawa ya kulevya.
TID amekuwa akihusishwa kutumia dawa kwa kipindi kirefu lakini ameendelea kukanusha.
Akiongea
kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds TV kinachoendeshwa na Kalapina,
Chief alisema TID ni msanii mwenye uwezo mkubwa hivyo ni muhimu kwa watu
kumshawishi kuachana na matumizi ya dawa hizo kama yeye alivyofanikiwa
kuacha.
TID
ni Q-Chief waliwahi kuwa maswahiba wa muda mrefu na walikuwa pamoja
kwenye Top Band japo walikuja kukosana. Hadi sasa hawaelewani na kauli
hii ya Q-Chief inaweza ikawa ni mwiba kwa Top in Dar!
Post a Comment