Featured

    Featured Posts

ROBIN VAN PERSIE ALA BATA ITALIA, STORI YA KUJIUNGA ROMA YAZIDI KUSHIKA KASI



Robin van Persie ameonekana akitembea huku na kule katika mitaa ya mji wa Rome nchini Italia.


Hali hiyo imeonekana kuzua gumzo kwamba huenda mshambuliaji huyo anaweza kutua AS Roma.

Van Persie alikuwa na mkewe Bouchra akipiga mitaa hali iliyosababisha baadhi ya vyombo vya habari kuamini huenda atahamia Italia.
 
Mkali huyo wa mabao kutoka Uholanzi amekuwa na msimu wa kubahatisha Manchester United, inakuwa ni lahisi sana kwake kuondoka.

Tayari kumekuwa na taarifa kwamba Roma walikuwa na mpango wa kumnasa Mholanzi huyo mwenye miaka 31. Hata hivyo, hadi sasa hakuna uhakika kuhusiana na hilo.




Post a Comment

www.CodeNirvana.in

.....


Powered by Blogger.

Translate

Total Pageviews

Copyright © HABARI ZA LEO | Designed By Code Nirvana