Mbunge
wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alijikuta kwenye
wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi wa jimbo lake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi wa jimbo lake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Hali
hiyo ilijitokeza jana asubuhi katika Kata ya Nshamba wilayani hapa
wakati msafara wa Kinana ulipofika kuzindua mradi wa maji. Kadhia hiyo
ilianza baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Ally Idd Ame kumkaribisha
mbunge huyo ili awasalimie wananchi.
Hata hivyo, wananchi hao walianza kuzomea kwa zaidi ya sekunde 40 wakipinga Profesa Tibaijuka kupanda jukwaani, hali iliyomlazimu Mkuu wa Wilaya, Francis Isack kupanda jukwaani na kutoa kauli ya kiutawala ili kuwanyamazisha wananchi hao.
Hata hivyo, wananchi hao walianza kuzomea kwa zaidi ya sekunde 40 wakipinga Profesa Tibaijuka kupanda jukwaani, hali iliyomlazimu Mkuu wa Wilaya, Francis Isack kupanda jukwaani na kutoa kauli ya kiutawala ili kuwanyamazisha wananchi hao.
“Anayetaka
kusikiliza abaki na asiyetaka aondoke,” alisema Isack na kuwanyamazisha
mamia ya wananchi hao. Baada ya kauli hiyo wananchi walitulia na
kuruhusu Profesa Tibaijuka kupanda na kuhutubia kwa muda.
“Kama hamnitaki siyo lazima niwe mbunge wenu, mnaruhusiwa kubadili. Huyo aliyewapa viroba asubuhi hii ili mje mnitie aibu mbele ya katibu mkuu wa chama nawaambia hiyo dhambi itawatafuna,” alisema.
Aliwaambia wananchi hao kuwa anachokifanya ni kuwatumikia na kuwaletea maendeleo, hasa
wanawake...
“Mimi
sitafuti kazi na wala sina njaa... na kama hela ya kula ninayo. Mimi
sigangi njaa na kama mnataka kuwa na kiongozi mganga njaa muwekeni muone
atawasaidia vipi,” alisema.
Akihitimisha
salamu zake kwa wananchi hao alisema kama wana jambo lao la ziada
walifanye lakini wamuache aendelee na jitihada za kuwaletea wanawake
maji... “Sina kinyongo na yeyote kwa sababu “I am too sophisticated (mstaarabu). Nipo juu ya mambo madogomadogo yanayowasumbua.”
Mbunge
huyo ambaye hivi karibuni aliondolewa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow, alimweleza
Kinana kuwa eneo hilo limekumbwa na upinzani kutoka kwa mtu anayehitaji
kulichukua ambaye ni kutoka ndani ya CCM.
Profesa
Tibaijuka alisema katika ubunge wake amefufua mradi huo wa maji
utakaogharimu Sh200 milioni kupitia shirika moja ambalo mkandarasi wake
ni wa Umoja wa Mataifa na utekelezaji umeanza miezi minne iliyopita
lakini unahujumiwa.
“Mradi
huu wa Nshamba unahujumiwa na wapinzani wangu kutoka ndani ya CCM na
vyama rafiki vya kisiasa, lakini lengo lao ni kunidhoofisha kisiasa,
jambo ambalo linadidimiza maendeleo,” alisema Profesa Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN – Habitat).
Kinana na kahawa
Katika
ziara hiyo, Kinana aliitaka Serikali mkoani Kagera kusimamia wakulima
kuuza kahawa ndani na nje ya nchi ili wanufaike badala ya kuwahusisha na
magendo.
Kinana
alisema wakulima wanahitaji kunufaika na kahawa yao kwa kuwa Serikali
haitoi pembejeo kwa zao hilo, hivyo wauze kahawa yao hata kama ni nje ya
nchi ilimradi wasivunje sheria
Alisema
Serikali haina budi kurekebisha sheria za uzalishaji wa zao la kahawa
zilizotungwa enzi za ukoloni inayotaja kuwa mkulima akizalisha zao la
biashara linakuwa ni mali ya Serikali, jambo ambalo ni kumnyanyasa.
Alivitaka
vyama vya ushirika kuepuka ukiritimba wa kutoa bei ndogo ya mazao ya
wakulima na kutaka wanapowachagua viongozi wa ushirika, waangalie walio
na uadilifu katika matumizi ya fedha.
Fedha za Mwenge
Akiwa
katika visiwa vya Bumbire na Mazinga, Kinana aliitaka Serikali
kusitisha uchangishaji wa fedha za Mwenge ambao hautawafikia wananchi,
akisema kitendo hicho ni kuwanyanyasa na kuwadhulumu.
“Uchangiaji
wa mafuta ya Mwenge ni wa hiari, si kuwalazimisha wananchi na
kusababisha Serikali kutoaminiwa na mkichangisha fedha hakikisha Mwenge
huo unafika kwa wananchi wa eneo husika,” alisema Kinana.
Aliitaka
Serikali ihakikishe inawalipa posho askari wake wanaoimarisha ulinzi na
usalama majini na nchi kavu badala ya kuwatoza fedha wananchi kuchangia
vyombo hivyo vinapokuwa vikitimiza majukumu ya kiserikali visiwani.
Post a Comment