Uongozi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), umesema utawafukuza kazi askari wote watakaojihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu ikiwamo kuwapiga raia wanaokosana nao mitaani.
Mkuu
wa Utumishi jeshini, Meja Jenerali Vicent Mritaba alitoa onyo hilo
mjibi hapa juzi alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya askari wapya
katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa la Oljoro.
“Jeshi
halitawavumilia askari wanaovunja sheria kwa kushiriki vitendo
vinavyokiuka maadili ikiwamo kujichukulia sheria mkononi,” alisema Meja
Jenerali Mritaba.
Alisema
jukumu la JWTZ ni kulinda mipaka ya nchi, raia na mali zao na kushiriki
kazi za kijamii kulingana na mahitaji ya wakati huo.
Pia
aliwaonya askari kutoshiriki wala kujihusisha na makundi maovu kwa
sababu itawaondolea sifa ya kuendelea kutumikia jeshi hilo lililoundwa
rasmi mwaka 1964, baada ya kuvunjwa jeshi lililorithiwa kutoka kwa
wakoloni.
Katika
hatua nyingine, Meja Jenerali Mritaba aliwataka wanajeshi wajiepushe na
vitendo vinavyoweza kuwasababishia maambuziki ya virusi vya Ukimwi.
“Mlipojiunga
jeshini wote mlipimwa afya zenu na kugundulika kuwa mpo salama. Epukeni
ngono kwa sababu mkipata maambukizi hayo ndoto zenu za kulitumikia
taifa zitakatika lakini pia malengo yenu ya kimaisha yatafifia,”
alisema.
Awali,
Mkuu wa Mafunzo ya Awali ya kijeshi katika Chuo cha Kihangaiko mkoani
Pwani, Kanali Ramadhani Churi alisema licha ya changamoto kadhaa
kiutawala, wahitimu hao wamefaulu katika hatua zote mbili za mafunzo
kuanzia ya wiki sita ya kuwaondoa kwenye hali ya kawaida kuwa wanajeshi.
Kanali
Churi alisema askari hao walifundishwa uvumilivu na kuishi katika
mazingira magumu ikiwamo kutolala kwa wiki sita mfululizo, lengo likiwa
ni kuwajengea uwezo kisaikolojia wa kuhimili jambo lolote gumu kwenye
uwanja wa vita na mapambano.
Kaimu
Kamanda wa Kikosi cha 833KJ Oljoro, Luteni Kanali Sijaona Myala alitaja
baadhi ya mambo yaliyofanikisha mafunzo hayo kuwa ni kila mtu
kuzingatia taaluma na kutekeleza wajibu wake kuanzia kwa wakufunzi,
madaktari na viongozi.
Post a Comment