Hakuna linalouma moyo kama mtu kuachana
na aliyempenda. Moyo husafiri kilometa nyingi kwa kuwaza. Hakukosea
aliyesema sikitiko la mahaba linashinda msiba. Lakini yote hayo yanaweza
kuepukika na kukaa mstari ulionyooka endapo mawasiliano
yatabeba umuhimu unaotosheleza na kusimama kwenyenguzo zake
kuu.MAWASILIANO: Ni nguzo kuu ya uhusiano. Ikiimarishwa huchochea amani
ya kudumu lakini kinyume chake ni kichocheo cha wapenzi kuachana. Ni
vizuri kujifunza lugha inayoweza kukufanya uelewane na mwenzako. Sauti
yako ukiwa mtaani itofautiane na ile ambayo unaitumia chumbani.Pengine
una kawaida ya kutoa majibu ya mkato unapokuwa unazungumza na rafiki zako,
lakini tabia hiyo hutakiwi kuizoea pale unapokuwa na mwenzio chumbani.
Ikiwa umezoea kuwaita wenzako: “Wewe!” Mwenzi wako hutakiwi kumwita
hivyo.Ni elimu ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwamba kutofautisha maeneo ni jambo
labusara. Kwamba sura yako iwe nyingine unapokutana na watu wa mitaani,
itofautiane unapokuwa na wazazi, vivyo hivyo pale ambapo upo sehemu
‘spesho’ na mwenzi wako.Lazima uwe unabadilika kama kinyonga. Ukiwa
kazini mbele
ya watu unaowaongoza unazungumza kwa sauti ya amri, lakini hiyo hupaswi
kuitumia unapokuwa na wazazi wako.Unaongea kwa sauti kali ya kuamrisha
mbele ya baba yako, hiyo adabu umefundishwa wapi?Kuna lugha ya
kuzungumza ukiwa na mwenzi wako. Ni mwiko kutoa sauti ya kuamrisha. Ni
vizuri kumnyenyekea lakini si katika kiwango ambacho kitakufanya
uonekane una kasoro za kisaikolojia. Tawile kwa kila linalosemwa na
mpenzi wako hairuhusiwi, unatakiwa kuweka mbele hisia zako.Upole
kupitiliza hauna maana kwamba wewe ni mpenzi sahihi. Eti, utaonekana una
nidhamu na unamsikiliza vizuri mwenzio, la hasha! Utatambulika kuwa mtu
hai kulingana na jinsi akili yako inavyofanya kazi. Namna hisia zako
zinavyoonesha uhai unapoguswa na matukio
mbalimbali ndivyo na ubinadamu wako unavyosomeka.Unahoji mambo kwa
sauti yenye ujazo wa kutosha, unachukia pale unapoona mambo hayajaenda
sawa, unaumia pale unapotendwa na unafurahi mipango inapokuwa chanya.
Hii ndiyo mantiki ya kukutaka uwe na akili hai. Itashangaza umepata habari kwamba mwenzi wako yupo gesti na mpenzi mwingine
halafu utabasamu.Sumu hatari inayosababisha mmomonyoko wandoa au
uhusiano wa kimapenzi kwa watu wengi ni kushindwa kujipanga kimaeneo.
Ratiba za ofisini kuingiza nyumbani. Marafiki kuathiri taratibu za
mapenzi yenu, ingawa kila kitu kina umuhimu wake kulingana na wakati
husika.Umeudhiwa na wafanyakazi wenzako kazini, unatakiwa kuweka hekima
mbele. Unarudi nyumbani ukiwa na imani kwamba huko utakutana na mwenzi
wako na ndiye mfariji wako. Kichwa kizito, basi mueleze mwenzio ajue
kinachokusibu kuliko kumpa majibu ya mkato. Itakuharibia badala ya
kukusaidiaNinachosisitiza hapa ni kuwa uhusiano wa aina yoyote
unadumishwa na mawasiliano.Lugha yako mbele ya mwenzi wako ina nafasi
kubwa ya kukufanya uendelee kufurahia penzi lake. Kinyume chake unaweza
kujikuta ni kero kwake. Atakuvumilia mwisho atachoka kwa sababu hujui
kubembeleza, unapenda kuamrisha.Unataka kuwa mtu bora kwenye uhusiano?
Zingatia chachandu zifuatazo:TAMBUA MAKOSA YAKOHii ni lugha nzuri mno
kwenye mapenzi. Unatakiwa kutambua makosa yako haraka na kutafuta njia
ya kusuluhisha. Ukijielewa kwamba umekosea halafu ukakaa kimya
hutoaishara mbaya mbele ya safari.KUWA
MWEPESI KUSEMA SAMAHANIKiingereza kinatawala sehemu kubwa ya
mawasiliano ya Watanzania, kwahiyo ukiona samahani utaonekana upo
kienyeji, basi sema Iam sorry. Hii ni baada ya kutambua makosa
naunapoomba msamaha umaanishe kutoka moyoni.USINUNE
AKINUNANi lugha ya mapenzi kwamba mwenzako akinuna, wewe jishushe ili
mpate muafaka. Nyote mkigoma mtafika saa ngapi? Ni kosa kubwa unapobaini
mwenzi wako ana hasira, nawe ukapandisha jazba kwani ni kiashiria
chakuachana.CHUKIA ASIYOYAPENDAInafundishwa kwamba rafiki wa rafiki yako
ni rafiki yako. Adui wa rafiki yako ni adui yako. Rafiki wa adui yako
ni adui yako. Adui wa adui yako ni rafiki yako. Falsafa hii ikupe somo
kwamba hutakiwi kupenda yale ambayo anayachukia.Haikubali mtu ambaye
hana jema kwa mwenzi wako, wewe umfanye rafiki. Fikiria upande wako
kwamba kuna mtu anakula yamini kukumaliza, halafu ugundue kwamba mpenzi
wako huwa anaketi naye na kuzungumza
kwa kugongeshana mikono? Heshimu hisia za mwenzako.ONGEZA MAPENZI KWA
ANAYOPENDAMapenzi ni sanaa, ukiweza kucheza karata zako mtadumu bila
kuchokana. Umeweza kuchukia yale ambayo hayapendi, sasa ni vizuri
kuongeza mapenzi kwa yale ambayo anayapenda. Hii itasaidia kuwafanya
muonekane ni kitu kimoja daima.Hata hivyo, iga kwa mambo mazuri, isije
ikawa mwenzako ni mtu wa baa kwa sana halafu na wewe umuige. Anapenda
siasa, mpe ushirikiano nawe uipende taratibu. Mpira nenda mkaangalie
pamoja, muvi na mengineyo, hayo ndiyo mapenzi.
MFANYE AKUTAMANI MUDA WOTENi rahisi, unapokuwa naye muoneshe mapenzi ya
dhati. Hakikisha hakasiriki mkiwa pamoja, yanayomhusu unabeba kama
yako. Humkaripiina unamfanya yeye ni bora. Msifie kwamba ni mzuri na
umueleze kwa hisia jinsi unavyomkubali. Hiyo itamfanya ajenge imani
kubwa kwako na ukiwa mbali atajiona pungufu.USITHUBUTU KUPAYUKAHata kama
mmegombana, linda sauti yako. Tumia hekima na myamalize kimyakimya.
SWEETHEART, DARLING, BABY, HONEY, DEAR
Mpe heshima yake na umuoneshe ni kwa kiasi gani alivyo na nafasi kubwa kwako. Usipende kumuita kwa kumtaja jina lake
au wengine wakishapata mtoto ndiyo utasikia “Mama Chausiku!” au “Baba
Semeni!”Haifai, tumia majina hayo au ukiweza tumia mengine yenye mvuto.
Ikupe raha kutamka na yeye imfanye afurahi kusikia kutoka kwako. Mapenzi
ni rahisi, utundu kidogo utakufanya uone dunia yote unaimiliki wewe.
Post a Comment