Zaidi
wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na kata ya goba jimbo la
ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma
ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja lao la muda
walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo
kusimama.
Wakazi
hao wamethirika zaidi kutokana na mto huo kufurika maji huku
ukiendelea kulika ukizifuata nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa wa
muungano waliopo kata ya goba na mtaa wa kilimahewa waliopo kata wazo
ambapo ITV imeshuhudia wakazi hao wakilazimika kuhatarisha maisha yao
kwa kutumia kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa ikiwa
inaninyinia katikati ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi wa
umeme nchini kakata huduma ya umeme katika kata hizo.
Wakizungumza
na ITV wakiwa wamefatana na mwenyekiti wao wa mtaa wa muungano wananchi
hao wamewalaumu vingozi wao wakiwemo wabunge na viongozi wa wilaya ya
kinondoni kwa kutowawekea daraja la kudumu katika mto huo na
kuwasababishia adha kila mara mvua kubwa inaponyesha ikwemo ya mwaka jana.
Wakazi
wengine waliokubwa na mafuriko ni wanaoishi kandokando ya mto mbezi
ambapo nyumba zao zimesombwa na maji huku kingo za mto huo zikiendelea
kulika na kufuata nyumba zao ambapo wameiomba serikali kuwapatia viwanja
vya bei raisi sehemu nyingine.
Katika
tukio lingine mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha visima vya
mafuta kujaa maji na kusababisha baadhi ya madereva wa vyombo vya moto
kukumbwa na adha kubwa ya magari yao kuzima baada ya kuwekewa mafuta
yalichanganyika na maji ya mvua katika kituo cha mafuta cha kobil
kilichopo afikana huku meneja wa kituo hicho akisuasua kuwalipa madereva
hao.
Post a Comment