Rais Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na Naseeb Abdul 'Diamond Platnum' alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam
RAIS
Jakaya Kikwete, ametoa mpya. Anasema kama asingekuwa Rais, huenda
angekuwa mwanamziki mashuhuri wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, kutokana na kipaji alichonacho.
Akihutubia sherehe za wafanyakazi jijini Mwanza leo, Kikwete alianza kwa kuimba kibwagizo cha wimbo wa “mimi msafiri bado niko njiani” ulioimbwa na mmoja wa wanamziki wa zamani, akisema matatizo ya wafanyakazi hao ni sawa na msafiri.
Ni katika kibwagizo hicho, Kikwete alijisifu akisema “kama sio urais pengine nami ngekuwa mwanamziki wa Bongo Fleva…maana sauti nzuri ninayo na niweza kuimba, japo nisingekuwa maarufu kuwapita akina Ali Kiba na Diamond (Naseeb Abdul).”
Kauli
yake iliibua vicheko uwanjani hapo, kuanzia viongozi waliokuwa wameketi
naye meza kuu hadi kwa maelfu ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.
Licha
ya Rais kufanya mzaha, lakini amekuwa mdau mkubwa wa sanaa ya mziki wa
kale na sasa, jambo ambalo amelipa msukumo mkubwa wakati wa uongozi wake
kwa kuwawezesha wasanii.
-chanzo:Mwanahalisi online
Post a Comment