ALIKO DANGOTE
Mtu tajiri barani Afrika Aliko Dangote
amesema kuwa bado anataka kuinunua kilabu ya Arsenal licha ya kushindwa kufanya
hivyo mwaka 2010 alipotaka kununua hisa za kilabu hiyo.
Bilionea huyo kutoka Nigeria ni tajiri mara nane ya alivyokuwa
wakati alipojaribu kununua hisa za klabu hiyo na kwamba shabiki huyo wa Arsenal
bado hajatupilia mbali ndoto yake ya kutaka kuinunua kilabu hiyo ya Landon
Kazkazini.
''Bado nina matumaini kwamba siku moja nitainunua timu hiyo','
alisema Dangote mwenye umri wa miaka 58.''Naweza kuinunua bei ambayo wamiliki
wake itakua vigumu kukataa'', huku akiongezea kuwa ''najua mpango wangu''.
UWANJA WA EMIRATES
La kushangaza ni kwamba Dangote ametaja hadharani kwamba Arsene
Wenger anafaa kubadilisha mbinu yake akisema kuwa timu hiyo inahitaji mwelekeo
mpya.
Dangote ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 ni tajiri zaidi ya
Stan Kroenke ambaye anamiliki hisa nyingi katika kilabu hiyo na Bilionea raia
wa Uzbek Alisher Usmanov ambao wamekuwa wakipigania udhibiti wa kilabu hiyo
katika miaka ya hivi karibuni
Post a Comment