KABAAANG!
Wakati supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitembea kifua mbele
huku akijinasibu kuwa anasubiri kwa hamu kupata mtoto kutoka kwa mchumba
wake, Zarinah Hassan ‘Zari’, imevuja picha inayomuonesha laivu mwandani
wake huyo akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi
ikidaiwa kuwa ni mtu wake wa nguvu, Ijumaa lina stori kamili.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Katunzi ni mtu
wake Zari kitambo kabla hata Diamond hajaanzisha naye uhusiano wa
kimapenzi mwishoni mwa mwaka jana na walikuwa wakikutana mara kwa
mara.“Katunzi na Zari walijuana kitambo sana. Yaani suala la Zari
kuibuka Bongo na kufanya mambo yao haikuwa ishu na hata Katunzi alikuwa
akiibuka Sauz (Afrika Kusini anakoishi Zari) na kuwa pamoja,” kilisema
chanzo hicho.
KATUNZI ALIWAKUTANISHA ZARI NA DIAMOND
Kuonesha kwamba kina ubuyu
kamili, chanzo hicho kilizidi kufunguka kuwa, hata safari ambayo
iliwakutanisha Zari na Diamond kwa mara ya kwanza, mrembo huyo alikuja
Dar, kumfuata pedeshee Katunzi, ndipo ‘dodo lilipomdondokea’ Diamond
kama kumsukuma mlevi vile.
“Kweli Diamond ana zari kama lilivyo jina la mrembo huyo mwenye asili
ya Kiganda. Siku hiyo ya kwanza kabisa walipokutana, Zari alikuwa
anaibuka Bongo kuitikia wito wa mtu’we Katunzi.
NDANI YA NDEGE SASA
”Diamond alichangamkia fursa, alipoona
‘dhahabu’ inaelea ndani ya ndege katika daraja la juu (business class),
akaomba namba, akakubaliwa na ndipo wakaanza kupiga mapichapicha ya
selfie ambayo yalivuja na Wabongo wakaanza kujiongeza kwani wakati huo
tayari Diamond alikuwa ameshaachana na Wema Sepetu ‘Madam,” kilitiririka
chanzo hicho.
PICHA ZAMSHTUA KATUNZI
Kwenye mazungumzo yake, chanzo hicho
hakikusita kufunguka kuwa baada ya picha za Diamond na Zari kuanza
kuvuja kwa mara ya kwanza, ilidaiwa kuwa zilimshtua Katunzi kiasi cha
kumtumia ujumbe mfupi wa simu Zari kumuuliza ni kitu gani kilikuwa
kikiendelea kati yake na mwanamuziki huyo.“Katunzi ilibidi amuulize Zari
kuhusu picha hizo, Zari akamwambia hakuna kitu chochote ni urafiki wa
kawaida, hata hivyo jamaa hakujali.
DIAMOND UPOOO!!
“Diamond kama aliingia katika himaya ya Zari
pasipo kujua kuna watu wanamjua kitambo atakuwa amechelewa. Pedeshee
Katunzi alimjua kitambo sana Zari,” kilimalizia chanzo hicho.
PICHA TOFAUTI ZANASWA
Mbali na kumwaga ubuyu huo, chanzo hicho
kilivujisha picha tofauti katika dawati la Ijumaa zinazomuonesha Katunzi
akiwa kwenye pozi la pamoja na Zari kuthibitisha kwamba wawili hao ni
watu wanaofahamiana.
KWA NINI URAFIKI WA SIRI?
Ijumaa lilifanya uchunguzi wa kwa nini
urafiki wa Zari na Katunzi ulikuwa wa siri na kubaini kuwa wawili hao
hawakutaka watu wajue kwa sababu ambazo wenyewe wanazijua lakini kitu
walichokuwa wanazingatia ni mpango wa ‘kula bata’.
Timu yetu ya
uchunguzi imebaini pia kuwa, wawili hao wamekuwa wakiwasiliana mara kwa
mara kupitia simu zao za mikononi, mawasiliano ambayo bado yanafanyiwa
kazi ili baadaye yapakuliwe yakiwa yameiva.
KATUNZI ANASEMAJE?
Baada ya kumsaka Zari bila mafanikio, mwanahabari wetu alimvutia waya
Katunzi ili kumsikia anazungumziaje ukaribu wake na Zari, alipopatikana
alijibu kwa kifupi.“Zari namfahamu, kuna nini kwani?” Alihoji Katunzi.
Alipoambiwa kuwa kuna picha na habari zake kuhusu Zari alikata simu na
hata alipopigiwa tena hakupokea.
KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Kufuatia kuwepo kwa minong’ono mingi
kuhusiana na ukaribu wa Zari na Katunzi, dawati la Ijumaa linaendelea
kuchimba undani wa habari hii kwa kumtafuta Katunzi, Zari na Diamond ili
wote wafunguke kwa kirefu.
Post a Comment