Mshiriki wa Big Brother Afrika ‘BBA’ Hot
Shot 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Munana, amemwagia sifa aliyekuwa
Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu kuwa ni mwenye mvuto wa kipekee.
Lakini licha ya kutoa sifa hizo,
mshiriki mwenzao
ambaye ndiye mwenyeji wao, Idris Sultan, hakutokea
katika sherehe hiyo jambo lililozua minong’ono kwa watu baada ya tetesi
kwamba ana ugomvi na Wema Sepetu.
Wema alimwagiwa sifa hizo alipokuwa katika sherehe za Instagram Party katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Wasanii ninaowakubali kutoka Tanzania
ni Wema Sepetu, ni mrembo sana nampenda, wasanii wengine ambao
nawakubali ni Shilole, Ommy Dimpoz pamoja na wimbo wake wa Wanjera,”
alisema.
Washiriki wengine wa BBA waliohudhuria sherehe hizo ni Nhalanhla na Samantha wote kutoka nchini Afrika Kusini.
Washiriki wengine wa BBA waliohudhuria sherehe hizo ni Nhalanhla na Samantha wote kutoka nchini Afrika Kusini.
Wasanii wa Tanzania waliohudhuria
sherehe hiyo ni Ben Paul, Izzo Bizness, Shelta, King Majuto, Stan
Bakora, JJ Band, huku mshereheshaji akiwa Adam Mchomvu, B Dozen na DJ
Ommy.
Hata hivyo, Wema alishukuru kupendwa na Luis. “Jamanii sina hata la kusema jinsi ulivyonisifia, nashukuru sana sana,” alijinadi Wema akishukuru.
Hata hivyo, Wema alishukuru kupendwa na Luis. “Jamanii sina hata la kusema jinsi ulivyonisifia, nashukuru sana sana,” alijinadi Wema akishukuru.
Mtanzania
Post a Comment