MKONGWE wa
filamu za mapigano kutoka Hollywood, Dolph Lundgren hivi karibuni
alijikuta katika wakati mgumu baada ya staa mwenzake wa kituo cha MTV,
Matthew Pritchard kumkojolea akiwa ndani ya ndege.
Matthew akiwa katika harakati za kumkojolea Dolph (aliyezungushiwa duara).
Tukio hilo lilitokea ndani ya ndege
binafsi iliyobeba mastaa hao wakiwa na watu wengine weng
i ambapo Dolph
pamoja na watu hao walikuwa wakitokea jiji la Amsterdam, Uholanzi kwenda
Marekani kuhudhuria mashindano ya mbio za magari yajulikanao kama
Gumball 3000 ambayo hufanyika Reno, Nevada.
Inasemekana kuwa Matthew alikuwa akinywa
kilevi kilichochanganywa na vidonge vya kulevya vij
ulikanavyo kama
Xanax na kumpelekea kuvua nguo zote na kupanda juu ya siti ya ndege na
kuanza kucheza wakati ndege hiyo ikitua katika bandari ya mji mkuu huko
Uholanzi.
Matthew akiwa
amesinzia baada ya kunywa vidonge hivyo.
Baada ya picha na vipande vya video hizo
kusambaa katika mtandao ya kijamii, Facebook, Matthew alivunja ukimya
na kusema;“Nilichukua Xanax ambayo niliamini itanifanya nilale nikiwa
ndani ya ndege.
“Sikujua kama itakuwa na madhara kama
ikichanganywa na kilevi. Nilikuwa nina kilevi sana mwilini. Nikaanza
kukimbia nikiwa ndani ya ndege utupu. Nikaanza kumkojolea Dolph miguuni
mwake.
“Baada ya hapo, Dolph alinishika mikono
yangu na kuniambia nisijali kwa hili lililotokea. Sijui
hata ni kwanini
sikuadhibiwa pale uwanja wa ndege.“Nilimuomba msamaha@dolphlundren na
amepokea msamaha wangu kama mtu mtanashati,” aliandika Matthew kwenye
ukurasa wake wa Twitter.
(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
Post a Comment