Featured

    Featured Posts

BAADA YA KUPIGIKA SANA,SIWEMA AMWANGUKIA NAY WA MITEGO!

Mwisho wa jeuri? Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson anadaiwa kumwangukia mwanamuziki huyo ili warudiane walee mtoto wao.

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni ndugu wa Siwema kilieleza kuwa, pamoja na  maneno ya shombo aliyommwagia Nay wakati wanaachana, mrembo huyo kwa sasa ameweka silaha chini akiomba wawe kama zamani.
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika pozi na Siwema Edson.
Kilidai kwamba hivi karibuni, mmoja wa dada wa Siwema (jina linahifadhiwa) amekuwa akimpigia simu Nay akimuomba arudishe moyo wake kwa Siwema, kwani tangu aachane naye mambo yamekuwa yakienda kombo ikiwemo ule msala wa kesi inayoendelea mahakamani ya kujipatia mali isivyo kihalali.
Ney wa mitego , Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilituma kijumbe kumfikishia Nay ombi hilo la Siwema ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Kweli nimepokea simu za msamaha. Nimemsamehe lakini siwezi kurudiana naye.”
Kwa upande wake mama Nay alisema yeye ndiye alikuwa mtetezi wake lakini kwa sasa hataki kusikia ishu hiyo

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

.....


Powered by Blogger.

Translate

Total Pageviews

Copyright © HABARI ZA LEO | Designed By Code Nirvana