*.Mabinti: Siri imeshafichuka na inavyoonekana wanasayansi tayari wameshafumbua
lile fumbo tata la nani mwoaji na nani mbabaishaji tu mtaka
uroda.*.Siku nyingine mpenziyo mpya akikuambia kwamba sababu yake kuu ya
kukupenda nimiguu yako, macho, kiuno, matiti, umbo namba nane au sababu zingine za kiumbo, kuna uwezekano mkubwa kwamba huyo njemba si mwoaji bali ni mtafuta uroda tu.*.Utafiti mpyauliofanywa katika Chuo Kikuu cha Texas, Austin
unaonyesha kwamba wanaume hutumia vigezo tofauti wanapotafuta
mwenzi.*.Kama lengo ni kutafuta mwenzi wa kudumu (mf. mke) basi wanaume
wengi hupendelea wanawake wenye sura nzuri lakini kama lengo ni uhusiano
wa muda mfupi tu (mf. kutimiza tamaa za ngono za muda mfupi) basi
wanaume wengi hutafuta wanawake wenye maumbo mazuri
wayatamaniyo.*.Watafiti hawa wamegundua kwamba, japo umbo ni muhimu
kidogo katika mahusiano ya muda mrefu, uso ni muhimu zaidi kwa sababu
ndicho kiashiria kizuri cha umri na “rutuba” ya mwanamke.*.Swali:Kuna
ukweli wo wote katika utafiti huu?Kinachonishangaza mimi ni kwamba suala
la tabiaya mwanamke - na hataNoeclexis-halitajwikabisa katika utafiti
huu, jambo ambalo nafikiri lilikuwa (na pengine bado) ni la muhimu
katika jamii nyingi za Kiafrika.
Post a Comment