Featured

    Featured Posts

TAZAMA HAPA VITUKO VYA BABY SHOWER YA AUNT EZEKIEL



VITUKO kibao vilitawala juzikati kwenye sherehe ya ujio wa mtoto wa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel  (Baby Shower), baada ya mastaa na waalikwa kibao kuonekana kufanya vituko vya hapa na pale.



Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akikata keki.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Mei 10, mwaka huu katika Viwanja vya Ndoto Polepole, huko Bagamoyo mkoani Pwani, ambako waalikwa walipata fursa ya kula, kucheza na baadaye kutoa zawadi kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa.
Aunt Ezekiel alimtambulisha mpenzi wake, Moze Iyobo kwa kumlisha keki kabla ya kumwagiana mabusu na kunyonyana ndimi hadharani.


Akimlisha keki mpenzi wake Moze Iyobo.
Licha ya tukio hilo, pia waalikwa walicheza vyema muziki kwa shangwe na furaha huku wakizungusha nyonga kwa ustadi wa aina yake.Waalikwa waliokuwa wamevalia sare za aina mbili, walikuwa burudani ya aina yake huku karibu wote, wakienda kulibusu tumbo la Aunt ambalo sasa limekuwa kubwa kiasi cha kuonekana kuwa ni mtu wa kujifungua leo au kesho.

Akiwa na mashost zake.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Aunt alisema anashukuru marafiki na ndugu zake kwa kuwezesha shughuli hiyo kufanyika, kwani awali aliamua aifanye baada ya mtoto wake kuzaliwa.“Nimefurahi sana maana watu wamejitolea kwa hali na mali na kubwa zaidi ni hii sehemu ambayo tumefanyia sherehe, kiukweli ni mbali sana hivyo inanifanya kuamini kila aliyeweza kuja huku ana mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Aunt.

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

.....


Powered by Blogger.

Translate

Total Pageviews

Copyright © HABARI ZA LEO | Designed By Code Nirvana