Hivi ndivyo unaweza kusema baada ya meneja wa mshambuliaji huyo wa kimataifa
wa Tanzania na TP Mazembe ya DR Congo, Jamal Kasongo kusema wameshakaa
na mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi kujadili juu ya kuuzwa kwa Samatta.
"Katumbi
anafahamu wazi kuwa Samatta kabikisha mwaka mmoja, aliniita juzi juzi
tu kujadili suala la mtoto (Mbwana Samatta). Muda mpekee kwa Katumbi
kutengeneza pesa ni majira ya kiangazi mwaka huu au majira ya baridi
mwezi januari mwakani, akishindwa hapo mwezi wa nne mwakani Mbwana
atakuwa mchezaji huru, ataondoka klabuni bure, Katumbi (Moise) hawezi
kukubali hilo".
"Kutokana na mazingira haya, suala la Samatta kwenda ulaya majira ya kiangazi mwaka huu halina ubishi, lazima aondoke".
Pia Kasongo amesema Samatta alishindwa kujiunga na CSK Moscow dirisha dogo la usajili
mwezi januari mwaka huu kutokana na kupata majeraha siku moja kabla ya
kucheza mechi ya kirafiki ambayo maamuzi yangetoka moja kwa moja.
"Katika
siku tatu alizofanya majaribio CSK Moscow alicheza vizuri mno, alifunga
magoli matatu, siku ya kucheza mechi ya kirafiki aliumia kifundo cha
mguu na hakutumika katika mchezo huo ambao ungetoa majibu. CSK wametoa
muda mwingi mrefu wa majira ya kiangazi kwa Mbwana (Samatta)".
Post a Comment