Adebayor ametupia picha hii Facebook na kuahidi kutoa sehemu ya 2 ya stori ya kaka yake Rotimi.
SAKATA la straika wa Klabu ya Tottenham ya nchini Uingereza, Emmanuel Adebayor
na familia yake limechukua sura mpya ambapo staa huyo ameahidi kutoa
sehemu ya pili ya stori 'ubuyu' mwingine kuhusu kaka yake mwingine
aitwaye Rotimi Adebayor muda muafaka ukifika.
Adebayor ameahidi kutoa ubuyu huo ikiwa
ni siku chache tangu aachie waraka wa kwanza kupitia ukurasa wa Facebook
uliokuwa ukielezea mambo anayofanyiwa na familia yake mbali na fadhila
nyingi alizowafanyia.
Katika waraka huo Adebayor alifunguka
mambo mengi akielezea anavyoibeba familia yake ambayo inaonyesha
kutobebeka na badala yake kumtupia lawama kuwa hana msaada wowote kwa
familia hiyo.
Kusoma waraka wa kwanza ingia: HAPA
Baada ya waraka huo, dada yake aitwaye
Lucia Adebayor aliibuka na kukanusha taarifa hizo akidai ni uongo mtupu.
Lucia aliandika hivi: "Lipo
wapi gari ulilodai kumnunulia mama....si ulilichukua....Nyumba unayodai
ulimnunulia dada ni uongo mtupu... Simu unazodai Rotimi aliiba nao ni
uongo....fedha siyo kila kitu ooooo...sisi wanafamilia hatukutaki tena
fanya mambo yako na sisi tufanye yetu.... kuwa nazo leo si kigezo cha
kuwa nazo pia kesho Mwenyezi Mungu akusamehe...uliwafukuza wapwa wako
ndani ya nyumba yako saa 6 usiku....Alpha na Mallams zimekuharibia
maisha yako. Unamhitaji Mungu.... Mungu pekee ndiye anayeweza kuokoa
roho yako." aliandika Lucia ambaye Adebayor ndani ya waraka
wake wa mwanzo alimuelezea kuwa amekuwa akiwaambia watu kwamba baba yake
alimwambia ampeleke Ulaya japo yeye hakuona sababu ya kumleta dada yake
huyo Ulaya maana kila mtu yupo huko kwa sababu flani.
Adebayor akiwa na mama yake mzazi.
Staa huyo ameandika kuwa stori hiyo ya
Rotimi itakuwa sehemu ya pili baada ya waraka wa mwanzo na kaka yake
huyo ndiye aliyemuelezea kwenye waraka wa kwanza kuwa alipokuwa Monaco,
alifikiria kuwa na familia ya wanasoka, hivyo akaamua kumpeleka ili
ajiunge na akademi ya soka huko Ufaransa japo ndani ya miezi michache,
kati ya wachezaji 27, aliiba jumla ya simu 21.
Mwaka jana Novemba, Adebayor aliibuka na
kuwatuhumu mama yake na dada yake kwa madai kuwa wanatumia uchawi
kumharibia kazi yake ya soka huku akikanusha kuwa hakumfukuza mama yake
huyo kwenye nyumba yake bali aliamua kuondoka mwenyewe.
Post a Comment