Featured

    Featured Posts

Nilimfuma Baba Akifanya Mapenzi Na Rafiki Wa Mama (NIAMBIE)

 

Mimi ni msichana wa miaka 19, Mwezi uliopita nilimkuta baba yangu akiwa anafanya mapenzi na rafiki wa mama yangu.Kipindi hicho mama yangu alikuwa hayuponyumbani, alikuwa hospitali kutokana na ajali aliyoipata, nami nilikuwa nahitajika kumpekekea chakula, ila wakati naenda ndipo nilipokumbuka kwamba nilisahau kutoka na hela kwa ajili ya kumnunulia mama maziwa na vitu vingine ambavyo aliniagiza.Hivyo nikaamua kurudi nyumbani na ndiponilipowakuta baba na rafiki huyo wa mama wakiwa wanafanya huo uchafu.Toka siku hiyo, baba yangu amekuwa ni mtu mzuri sana kwangu, kwa maana amekuwa akininunulia vitu vingi na vizuri ilitu nisiseme chochote kwa mama, na kiukweli nimekuwa nikikataa kila alichonipa, kwa maana niliamini kwamba ni katika kutaka kunipumbaza.Swali langu ni kwamba, mnafikiri ni vyema kwa mimi kumwambia mama yangu, kiukweli nisingependa wazazi wangu watengane na pili, nafikiria kwamba huenda baba na yule mwanamke ambaye ni rafiki wa mama wanaendeleza mcheza wao.Mama yangu kwa sasa yupo nyumbani na anaendelea kujisikia vyema, ila nachanganyikiwa kama kweli nahitajika kumwambia.Kwa mtakao nishauri naomba msimtukanebaba yangu, najua alisaliti ILA NIPO HAPA KWA AJILI YA USHAURI, SINA MTU WA KUONGEA NAYE, NIMEZAZLIWA PEKE YANGU NA NAWAPENDA MAMA NA BABA YANGU SANA.NISAIDIENI TAFADHALI......

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

.....


Powered by Blogger.

Translate

Total Pageviews

Copyright © HABARI ZA LEO | Designed By Code Nirvana