Wananchi wakiwa wametaharuki katika eneo la Ubungo kutokana na mgomo unaoendelea.
Polisi wakijaribu kuwasihi baadhi ya madereva kuacha mgomo.
Mabasi yakiwa yamepaki ndani ya Kituo cha Mabasi Ubungo.
Baadhi ya abiria wakionekana kutafakari juu ya safari yao katika Stendi ya Ubungo.
Baadhi ya abiria wakiwa wamekata tamaa ya safari na kuamua kurudi nyumbani.
Hali halisi ya Stendi ya Ubungo.
Taswira nzima ya mabasi yaendayo mikoani katika Stendi ya Ubungo.

Elisha Waziri, mkazi wa Kimara-Mwisho akizungumza na mwanahabari wa Global TV Online, Melkiadi Oreje.
Mmoja wa abiria akilazimika kupanda Bajaj ili kumfikisha eneo lake la kazi.
Mmoja wa abiria akilazimika kupanda Bajaj ili kumfikisha eneo lake la kazi.
KWA mara nyingine mgomo
wa mabasi yaendayo mikoani na mabasi madogo (daladala) jijini Dar
umeibuka na kuwafanya wananchi watumiao usafiri huo kubaki katika hali
ya sintofahamu kwa kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.
Mgomo huo umechukua sura mpya baada ya
madereva kudai kuwa serikali imekiuka ahadi waliyopewa na Waziri wa Kazi
na Ajira, Gaudensia Kabaka kuwa hawatasoma kila baada ya miaka mitatu
pindi wanapotaka kuhuisha leseni zao.
Mbali na madai hayo, madereva hao
wameweka mgomo kwa kigezo cha kushinikiza waajiri wao wawape mikataba ya
kudumu. Mwandishi wetu amezunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na
kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya mikoani pamoja na daladala
zikiwa hazifanyi kazi.
Mwanahabari wetu aliyeambatana na Timu
wanahabari wa Global TV Online, alifika eneo la Stendi ya Kimara-Mwisho
na kukuta wananchi wakitumia usafiri bodaboda na Bajaj kwenda katika
sehemu zao za kazi huku baadhi yao wakieleza usumbufu mkubwa walioupata
kutokana na mgomo huo.
“Kimsingi sisi wananchi mgomo huu
unatuumiza zaidi. Mimi nafikiri wahusika wa pande zote mbili wanapaswa
kuchukua hatua za haraka ili kutunusuru sisi tunaotumia usafiri huu
lakini pia uzalishaji wa taifa,” alisema Juma, mkazi wa Kimara-Mwisho.
(PICHA STORI / DENIS MTIMA / GPL)
Post a Comment