BALAA LA WAJAWAZITO KUPENDA CHIPSI KUKU
Hamida Hassan
Ugonjwa unaowakabili watoto waliotoka mgongo nje pamoja na vichwa vikubwa, unaelezwa kusababishwa na ukosefu wa Folic Acid mwilini, hali inayochangiwa na mama mjamzito kupenda kula chipsi kuku.Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wodi ya watoto ya Moi, Agricore Joseph alisema wanawake wengi hufikia hatua ya kujifungua watoto wenye matatizo hayo kutokana na kupenda vyakula hivyo, kitu ambacho kinaweza kuepukika.
Mtoto aliyezaliwa akiwa na kichwa kikubwa.
Dokta Agricore aliyasema hayo alipokutana na MC maarufu jijini Dar, Joyce Amina Mwakipunda ‘Mc Jojo’ na Mtangazaji wa Kipindi cha Tashtiti Zetu cha Redio Uhuru, Nuru Issa, walipofika hospitalini hapo kutoa misaada mbalimbali kama vile pampasi, mafuta, poda, maji ya kunywa, juisi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yao ya kuzaliwa.
Mtoto akiwa na uvimbe mgongoni.
“Nakujua wewe ni MC maarufu, huko unakopita jaribu kuwaelimisha wanawake juu ya tatizo hilo, na wewe Nuru kwenye kile kipindi chako waelimishe wanawake juu ya hili, naamimi tunaweza kupunguza idadi ya wanaojifungua watoto wenye tatizo hili,” alisema daktari huyo.Alisema, ni wakati sasa wanawake hasa wajawazito kuelimishwa juu ya kutopendelea chipsi kuku badala yake kutumia vyakula ambavyo vinaongeza Folic Acid na kunywa vidonge vinavyotolewa kliniki
Post a Comment