Kajala Masanja akiwa na bandeji kichwani baada ya kupigwa chupa.
STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja,
kupitia akaunti yake ya Instagram hivi punde amesema maisha yanaendelea
ikiwa ni siku mbili baada ya kupigwa chupa na mtu asiyemfahamu usiku wa
kuamkia Jumatatu akiwa klabu wakati alipokwenda katika shoo ya
kumchangia mke wa Mabeste, Maisha Club.
Kajala akiwa Maisha Club kabla ya kujeruhiwa kwa chupa.
Kajala alieleza kuwa tukio hilo
lilitokea wakati akijiandaa kutoka Maisha Club ambapo ghafla akiwa
kwenye ngazi alirushiwa chupa kichwani iliyopelekea kuanguka kutoka
kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na wasamalia wema waliompeleka
Hospitali ya Mwananyamala ambapo alishonwa kwenye jeraha alilolipata.
Staa huyo aliongeza kuwa mtu aliyempiga
chupa ni mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio
hilo alikuwa hamjui na wala hajawahi kumuona mtu huyo.
Post a Comment